Taarifa za uhakika ni kwamba kweli mwigizaji Sajuki amefariki dunia leo asubuhi (jan 2 2013) katika hospitali ya Muhimbili.
Alilazwa hapo kwa wiki mbili
ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye
matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena december 2012.
Dinno ambae ni rafiki wa karibu
wa Sajuki ameniambia kwamba tatizo kubwa lililomzuia
Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye
huduma ya gesi.
Baada ya kuhangaika sana,
dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa
huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio
lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.
Sajuki alikua na tatizo kubwa
la kupumua wakati huu ambapo Dinno amethibitisha kwamba upumuaji wake
ulikua unabadilika mara kwa mara.
Msiba upo Tabata,
Mwenyenzi Mungu amlaze pema Sajuki.
No comments:
Post a Comment