Izzo amesema “hii single inaitwa ‘MWAKA JANA’ na nimezungumzia mambo ambayo yalitokea mwaka jana ambayo yalinigusa, ni mwaka ambayo sikuupenda sana likiwemo la baba kupata kesi kubwa ambayo kama angeshindwa angefungwa jela kwa muda mrefu tu na ilinifanya niache chuo kwa muda”
“Jingine ni ajali kubwa ya Five Stars, kifo cha Mr Ebbo, ishu ya Waziri Mwakyembe kulishwa sumu, Diamond alimvisha pete Wema Sepetu, Marlow alimuoa Besta, kifo cha Osama majonzi mpaka leo…. hii ni bonge la idea ni bonge la track” – Izzo B
Kwenye sentensi nyingine Izzo B amesema beat ya hiyo single alihamishiwa kwenye simu na producer Maneck wakati wamekutana washiriki wa KTMA 2012 lakini hakumwambia kwamba angempa beat lakini baadae akampatia na kazi ikafanyika.
No comments:
Post a Comment