MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye alikuwa afanye onyesho maalumu katika ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam leo, amesitisha kutokana na janga la milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana jijini Dar es Salaam jana, msanii huyo amefikia uamuzi huo
kwa masikitiko hadi hapo baadaye itakapotangazwa tena.
“Nasikitika kuwajulisha kuwa, kutokana na maafa ya mabomu yaliyotokea Gongo la Mboto, Dar es Salaam hatutakuwa na ‘concert’ yetu kesho (leo), Mungu awalaze mahali pema marehemu wote na kuwajalia afya njema majeruhi wote,” alisema Sugu katika taarifa yake.
Katika onyesho hilo, Sugu alipanga kutumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na mashabiki wake ambao walimuunga mkono katika harakati zake za kuwania ubunge.
Wasanii wa kundi la Orijino Komedi, Salu T, Fred Maliki ‘Mkoloni’ walipangwa kumsindikiza Sugu au ukipenda Mr II, katika onyesho hilo.
na Elias Charless.
No comments:
Post a Comment