Ray c she iz beutifullly?..

Si nyingine bali ni ile Kampuni ya utengenezaji wa Filamu na Tamthilia hapa nchini ya Tuesday Entertainment ya jijini, inatarajia kufyatua Filamu yake mpya ijulikanayo kama Beautiful.
Filamu hiyo ya Beautiful itafyatuliwa wiki ijayo na kusambazwa nchini nzima, kwani imesukwa Mkoani
 Morogoro

na inatarajia kuwashika wapenzi wa filamu wa hapa nyumbani Bongo kulingana na ubora wa Filamu yenyewe kuanzia upigaki na hata hadithi.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mr. Chuzi amesema kuwa filamu hiyo, imemchukua muda mrefu kwenye maandalizi kwa ajili ya kufanya utafiti na kuchagua wasanii ambao wanaendana na hadithi yenyewe ili kuleta uhalisia na kutoa elimu ikiambatana na burudani kwa watazamaji anaelezea Mr. Chuzi.

Anaweza sema Filamu hiyo ni Lulu kwa sababu ametumia muda mwingi kumtafuta msanii ambaye alimuhitaji kwa ajili ya Filamu hiyo.

Hatimaye anakutana na msanii nyota na Gwiji kwenye masuala ya sanaa, lakini si ya kuigiza bali ni muziki si mwingine bali ni Binti Rehema Chalamila ( Ray C) na anamudu kuigiza kama yupo kwenye game kwa kipindi kirefu na ameweza kufanya vyema kwenye hiyo Movie.

Wasanii wengine walioshiriki kwenye Filamu hiyo ni pamoja na Rehema Chalamila aka Ray C kiuno bila mfupa ni Charles Magari, (Mzee Magari), Asnat, Nyanda Mr. Chuzi na wasanii wengine wangi wakali katika game hili. Filamu hii inasambazwa na kampuni ya Steps Entertainment nchi nzima.

No comments:

Post a Comment