Alianza kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumanne iliyopita kuhusu kuachana na Shyrose bila kutaja sababu lakini siku tatu baadaye alimtaja Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuwa chanzo.
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda lina ‘full story’ kuhusu skendo hiyo baada ya kukusanya ‘data’ kutoka kila upande.
UKWELI ULIOFICHIKA
MOSI: Jaffarai alipozungumza na gazeti hili Ijumaa iliyopita alisema kuwa inamuuma kuachana na Shyrose kwa sababu walikuwa kwenye mkakati wa kupata mtoto.
“Tulipanga tangu mwezi uliopita lakini ikashindikana, mwezi huu tukaweka malengo mengine. Ndoto hiyo imekwenda na maji. Haiwezekani kupata mtoto tena na Shyrose,” alisema Jaffarai.
PILI: Ni majuto kwa Jaffarai, kwani katika mazungumzo hayo yaliyochukua nafasi katika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam staa huyo wa ‘Nipo Bize’ alisema:

“Najutia muda wangu. Nimekaa na Shyrose kwa miaka nane lakini hakuna faida niliyopata. Nilichovuna ni ulevi na kuvuta sigara.”
TATU: Fedha ndiyo iliwaunganisha? Jaffarai anafunguka: “Hili wengi hawalijui, nimekuwa na Shyrose tangu akiwa anafanya kazi TVT (sasa TBC1), hakuwa na fedha.
“Mimi nilikuwa nafanya muziki, napata fedha na tukawa tunasaidiana lakini baadaye alibadilika na kuwa na kipato kikubwa kuliko mimi.”
NNE: Vipi life style (mtindo wa maisha) yao? Jaffarai alisema: “Kwa starehe ilikuwa mambo poa. Shyrose alikuwa anaweza kugharamia chochote tulipotaka ‘kula bata’.”
TANO: Maumivu ambayo Jaffarai amekiri yanamtesa ni haya: “Inabidi kuanza upya kwa sababu mipango mingi niliiahirisha. Nilitaka kujiunga na chuo kikuu hapa Dar, Shyrose akaahidi kunilipia ada Marekani.
“Yote hayo hayakufanikiwa. Mimi kama mwanaume nina mipango yangu ya kimaisha, kwa hiyo najipanga upya kimuziki.”
JAFFARAI APEWA SOMOHaya ni baadhi ya maoni ambayo marafiki wa Jaffarai walimtumia kwenye ukurasa wake wa Facebook.
JESSY ISMAIL: Pole Life Goes on don’t give up, songa na maisha and make a difference after all hakuna life forever. Make use of your talent and prove that you are better than most Cheers bro, keep your chin up!
PIUS MBAWALA: Veve manywele iko chezea Sugu veve.
LUCAS EDWARD: Inaonekana imekuuma sana kaka!?
DORAH KIWALE: Too bad! Pole sana!
ZUBERI SIRAJI: Ukimegewa demu wako, tafuta mnyonge ummegee, haipunguzi maumivu ila inarudisha hadhi ya kiume.
FRANK PAUL: Lakini mtu mzima haikupaswa kuongelea issue yako kiuwazi namna hiyo, pia yule alikuwa ni dem wako 2 hivyo alikuwa free kwa lolote. Uliposema wewe na huyo dada mmeachana ilikuwa inatosha sana na hukutakiwa kufikia hapo ulipo ktk kuelezea... that why watoto wa kiume tukapewa koromeo.

LUQMAN SAID: Katika maisha kuna kusameheana kama mmoja amekwenda kinyume. Jeff nakuomba usiwe na hamaki, vumilia Inshallah Mola atakujalia utapata wako mwingine ila ninalokuomba usimseme tena kwa ubaya, hakuna mkamilifu.
NGENDAHEKA DAUD: Najua upo katika wakati mgumu sana, ila kinachotakiwa siyo kukimbia tatizo bali kukabiliana nalo, na matatizo ndiyo yanayokomaza, samehe saba mara sabini, kuwa mpole angalia mbele, hakuna sababu ya kuweka beef na Sugu, maisha yapo tu.
HABARI CHINI YA CARPET
Data za kuaminika zinaweka wazi kuwa alichokifanya Jaffarai ni kumkomoa Shyrose na Sugu kwa sababu wachumba hao ‘walimwagana’ siku nyingi zilizopita.
“Wale walishaachana na kuna magazeti yaliripoti. Walikuwa pamoja kwa sababu za kirafiki, inaonekana Jaffarai ameamua kumchafua Sugu,” alizungumza rafiki wa wachumba hao na kuongeza:
“Nazungumza kama mtu wa karibu na Jaffarai pamoja na Shyrose, wawili hao waliachana zaidi ya mwaka sasa, nimeshangaa leo kusikia Jaffarai analaumu, inaonekana anataka kumharibia Shyrose.
“Naomba Jaffarai awe mkweli na aangalie asitumiwe. Inawezekana kuna watu wana chuki na Sugu, kwa hiyo wanaona wamtumie Jaffarai kumchafua bila kujua wanamuumiza pia Shyrose.
“Shyrose alikuwa mwanamke huru, kwa hiyo hata akiwa na Sugu hakuna ubaya. Shyrose siyo mke wa mtu, Sugu siyo mume wa mtu. Hakuna tatizo, nashangaa huyo mtu anayemfadhili Jaffarai mpaka kwenye vyombo vya habari ili kuwachafua.”

Hata hivyo, Jaffarai alipoulizwa hilo alijibu: “Mimi na Shyrose tulikuwa hatujaachana na ndiyo maana tukawa na mipango ya kupata mtoto na akawa ananisisitiza tuoane.”
SHYROSE AJIPANGA
Gazeti hili lilimtafuta Shyrose bila mafanikio lakini mtu wake wa karibu alisema: “Kumpata ni ngumu. Hivi sasa anajipanga upya, anahitaji kuhurumiwa. Alichokifanya Jaffarai kimemuumiza sana.
“Watu wanaachana na wanasameheana. Uadui hauna maana. Alichofanya Jaffarai hakijengi. Tunaomba kwanza muda wa kumfariji Shyrose.”
VIPI SUGU?
Jitihada za kumtafuta Sugu anayekula ‘shavu’ kama mwasisi wa Bongo Fleva ziligonga ukuta lakini mtu wake wa karibu alijibu:
“Hakuna kitu ambacho Sugu anaweza kuzungumza hapo.
Hana muda wa kuzungumzia vitu binafsi ila muda wake anauelekeza kuwatumikia wananchi wa Mbeya na ukombozi wa Bongo Fleva.”
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Jaffarai ni mtu maarufu kama ilivyo kwa Shyrose. Ingekuwa vema suala hili likazungumzwa na kumalizwa nje ya vyombo vya habari.
Hatua iliyochukuliwa na Jaffarai inaweza kuwafanya watu waamini kuwa anatumiwa na wenye uhasama na Sugu
Ikumbukwe kwamba hivi sasa Sugu anasuguana na baadhi ya watu akidai malipo ya Mradi wa Malaria Haikubaliki ambao aliuanzisha na kuutafutia wafadhili kabla ya kibao kugeuzwa na kupewa mtu mwingine.
Tunamuomba Jaffarai aache jazba na kuchukua uamuzi wa pupa katika kipindi hiki ambacho ana hasira, kwani hasira hasara.
Kwa upande wa Shyrose tukio hili lichukuliwe ni somo kwake, kama kuna kosa alilofanya katika kipindi chote cha uhusiano wa kimapenzi na Jaffarai awe amejifunza na asirudie kosa.
Anatakiwa kuwa jasiri na mwenye subira katika kipindi hiki kigumu ili asipoteze mwelekeo na mipango ya maisha yake ya baadaye.
No comments:
Post a Comment