Baba ake hemedi Kufariki Dunia.

Anga la burudani likifunikwa na kifo cha msanii, Dalila Peter Kisunde ‘Tabia’, staa wa filamu, Hemed Suleiman (pichani) amepata pigo kubwa kwa kuondokewa na baba yake mzazi, Suleiman Hemed.

Kwa mujibu wa Hemed, baba yake alifariki dunia Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Tanga na kuzikwa siku iliyofuata baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kisukari.
“Alifariki wakati natoka Tanga kumwona narudi Dar kwa sababu ni muda mrefu alikuwa anaumwa. Nilipofika Kibaha nilipokea taarifa kwamba amefariki, kwa hiyo nilibadilisha gari, nikarudi Tanga msibani,” alisema Hemed.
Inna Lillah Wainna Ilayh Rraj’uun.

No comments:

Post a Comment