Album mpya THT

UZINDUZI wa albamu sita za wasanii wa Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania ‘Tanzania House of Talents’ (THT), uliofanyika usiku wa kuamkia Januari 12, ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ulikuwa wa aina yake,

Sherehe hizo zilizokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo zilihudhuriwa na watu wapatao 400 wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa na Waziri wa Vijana, Habari na Michezo, Mhe. Emmanuel Nchimbi.
Kwa upande wa shoo, wasanii waliozindua albamu zao na majina ya albamu kwenye mabano, Estelina Sanga ‘Linah’ (Natamani), Ally Mataluma (Mama Mubaya) Barnaba Elias (Kichwa Changu), Amini Mwinyimkuu (Yameteka Dunia), Mwasiti  Almas (Kamili) na Lameck Ditto (Wapo) walionesha uwezo wa hali ya juu wa kuimba huku kila mmoja akitumia staili ya aina yake kuteka hisia za watu.
Aidha, wasanii wengine waliosindikiza uzinduzi huo ni pamoja na Laurence Malima ‘Marlaw’, Banana Zorro na Maunda Zorro ambao nao walitoa shoo zilizoifanya shughuli hiyo ifane zaidi.
Niliweza kushuhudia kazi ya msanii mmoja baada ya mwingine hivyo kuweza kutoa ‘maksi’ kwa kila mmoja kutokana na namna alivyoweza kulitawala jukwaa na kutoa burudani iliyostahili.
Kwa tathmini hiyo, Mwasiti, Ditto na Mataluma walipata nane kwa kumi, Maunda na Banana waliopata saba kwa kumi, Barnaba na Marlaw; sita kwa kumi huku Linah, Pipi na Amini wakiambulia tano kwa kumi.
Kwa upande wa nyimbo, Kariakoo wa Mataluma, Nalivua Pendo na Siyo Kisa Pombe za Mwasiti, Bora nikimbie wa Linah ni kati ya zile zilizowashika zaidi wadau wa muziki ambapo baadhi walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakiamka kucheza.

No comments:

Post a Comment